Hayo yamesemwa Bungeni na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe wakati akiuliza swali kwa serikali juu ya uamuzi wa serikali kuvifanya viwanda vilivyokuwa vinabangua korodho kubakia kuwa maghala ya kuhifadhia nafaka huku korosho zikipelekwa nje kwenda kubanguliwa na kwenda kuzalisha ajira kwa watu wengine huko.
Kwa upende wa waziri mwenye dhamana ya viwanda na Biashara na uwekezaji Charles Mwijage amesema kuwa serikali tayari imekwishatoa agizo kwa wawekezaji wote ambao walikabidhiwa viwanda vya umma kwa lengo la kwenda kuviendeleza na wakageuza matumizi wavirudishe serikalini au waanze uzalishaji mara moja.
''Seikali inatambua umuhimu wa zao hilo na upatikanaji wa ajira kama korosho zote zitabanguliwa hapa nchini ,na tayari nimekutana na mwekezaji toka India atajenga kiwanda kikubwa sana kitakachobangua korosho zote na kuleta ajira kwa vijana wetu''. Amesema waziri Mwijage




