Tuesday , 14th Jul , 2015

Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tacaids imesema makundi ya vijana na wanawake wenye umri kuanzia mika 30 hadi 34 ndio yanayoongoza kwa kuwa na Virusi vya Ukimwi(VVU).

Mwenyeikiti wa Taifa wa tume ya kudhibiti ukimwi ya TACAIDS Bi Fatma Mrisho

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Bi. Fatma Mrisho alipokua anazumgumza na wanaharakati waliopanda na kushuka mlima kilimanjaro ili kukusanya fedha za mapambano dhidi ya Ukimwi.

Dk. Mrisho amesema kuwa pamoja na kupungua kwa maambukizi ya UKIMWI kutoka asilimia 5.7 hadi 5.1 kwa mwaka 2011 na 2012 takwimu zinaonesha ongezeko kubwa la maambukizi kwa vijana na wanawake watu wazima.

Kwa upande wake Makamu Rais wa Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu Geita Gold Mine, Simon Shayo amesema wamejitokeza kushirkiana na TACAIDS ili kukusanya fedha zitakazowezesha kutokomeza ugonjwa huo hapa nchini.