Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
Akiongea mara baada ya matembezi ya hisani ya kuchangia fedha za kuwasomesha wauguzi wakunga iliyofanywa na shirika lisilo la kiserikali la AMREF Tanzania, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema, serikali inafanya jitihada nyingi kupunguza vifo hivyo kwani ni hatari kwa ukuaji wa na maendeleo ya Taifa.
Aidha. Mhe. Ummy amesema, serikali imeongeza bajeti ya Afya kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ili kuweka miundombinu bora ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, kusogeza karibu Zahanati katika kila kijiji na kila kata ili kupunguza msongamano katika hosptali za wilaya sambamba na kutekeleza mkataba wa Abuja wa kutenga bajeti ya afya kwa asilimia 15 ya bajeti yote ya nchi.
Ameongeza pia kuwa mpango wa serikali ni kupunguza vifo vya wanawake kutoka 432 hadi 200 ifikapo mwaka 2020.
Naye, Mwakilishi Mkazi wa AMREF Tanzania Dkt. Florence Temu amesema lengo lao la kusomesha Wauguzi Wakunga 400 ni kupunguza upungufu mkubwa wa Wakunga Wauguzi katika vituo vya afya hasa maeneo ya vijijini ambapo amesema kiasi cha shilingi millioni 500 kitafanikisha kusomesha wakunga hao.
Kwa mujibu wa Waziri Ummy, Tanzania ina upungufu wa wahudumu wa sekta ya afya kwa asilimia 48, na kwa upande wa wauguzi wakunga, waliopo ni 25,216 huku mahitaji yakiwa 37,741