Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza kwa nyakati tofauti katika Wilaya za Chemba na Kondoa ambapo amezunguka kuangalia namna zoezi la kuunda madawati linavyoendelea.
Mkuu wa wilaya ya Chemba Ramadhani Maneno amemueleza Mkuu wa Mkoa kwamba Wilaya yake ina upungufu wa madawati 9,400 ambapo hadi sasa wameshatengeneza madawati 5000 huku mengine yakiendelea kutengenezwa.
Aidha Wilaya ya Kondoa Mkuu wa Wilaya Shaban Kisu amesema kwamba ina upungufu wa madawati 10580 ambapo hadi sasa wameshatengeneza 2,999 na kazi ya kumalizia mengine inaendelea.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Rugimbana amewataka wilaya za mkoa wake kushirikiana hasa zile zinazotoa mbao kuhakikisha wanawezesha upatikanaji wa mbao ili zoezi hilo lifanikiwe kwa ufanisi.