Afisa Elimu wa mkoa wa Mtwara, Fatuma Kilimia, akielekezwa na wanafunzi matumiz ya tehama
Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, afisa elimu wa mkoa wa Mtwara, Fatuma Kilimia, amesema magari waliyopatiwa halmashauri hizo yatasaidia kurahisisha ufuatiliaji wa masuala ya taaluma katika maeneo mbalimbali hasa ya vijijini ambako miundombinu yake sio mizuri.
Naye, meneja wa mradi huo, Felix Mbogela, amesema kumekuwa na mafanikio makubwa tangu mradi huo ulipoanza, na kwamba kwamujibu wa utafiti uliomalizika mwezi Novemba mwaka huu, idadi ya watoto wasiojua kusoma na kuandika imepungua kutoka asilimia 69 mpaka kufikia asilimia 25.
Mradi huo ambao umefikia mwisho baada ya kufanya kazi kwa miaka mitatu toka ulipozinduliwa mwaka 2012, umesaidia kuinua kiwango cha elimu mkoani humo pamoja na watoto wengi kuhamasika kupenda kusoma kutokana na aina ya ufundishaji inayotumika kupitia Kompyuta.