Kaimu mkurugenzi wa mazingira ofisi ya makamu wa Rais nchini Tanzania Bw. Richard Mayungi amewataka watanzania kutambua kwamba sasa siku ya jumamosi ya kila mwisho wa mwezi imeshatengwa kisheria kwa ajili ya kila mwananchi kushiriki usafi wa mazingira kuanzia saa 12 asb hadi saa 4.
Amesema kwa yule ambaye hatashiriki atachukuliwa hatua kwa mujibu wa maelekezo ya kisheria yaliyotolewa na tayari wameshaanza kuwafikisha mahakani wafanyabiashara ambao wamefungua maduka yao huku wakitambua kwamba ni siku ya kushiriki usafi wa mazingira.
Amesema ofisi yake itakwenda nchi nzima kutoa elimu kwa wananchi juu ya sheria hiyo ili waweze kushiriki kikamilifu kufanya usafi ambao utawasaidia pia kuepukana na magonjwa ya milipuko.





