Saturday , 5th Nov , 2016

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR lina wasiwasi mkubwa kuhusu hatma ya msemaji wa Riek Machar nchini Kenya, James Gatdet Dak ambaye alipewa amri ya kuondoka nchini humo tarehe pili mwezi huu kurejea Juba, Sudan Kusini.

Msemaji wa Riek Machar,(Kushoto),Bw. James Gatdet Dak

Katika taarifa yake, UNHCR imesema hofu hiyo inazingatia kuwa Bwana Dak alishapatiwa hadhi ya ukimbizi nchini Kenya na kwamba kitendo cha kulazimishwa kuondoka ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa za ukimbizi.

UNHCR imesema jitihada za kuomba serikali ya Kenya kubadili uamuzi huo hazikuzaa matunda na hivyo walichofanya sasa ni kuisihi serikali ya Sudan Kusini ihakikishe haki za binadamu za Bwana Dak zinazingatiwa.