Umati wa wakazi wa Temeke katika tamasha la siku ya maadhimisho ya Kimataifa ya Vijana Duniani
Takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani UNFPA tawi la Tanzania zinaonesha kuwa ni asilimia 17 tu ya vijana wote walio na umri wa zaidi ya miaka 18 ndio wanaotumia uzazi wa mpango jambo linalosababisha kuwepo kwa ongezeko la watu nchini.
Akiongea leo Jijini Dar es salaam, Mwakilishi Msaidizi wa UNFPA nchini Tanzania Dkt. Rutasha Dadi, ametoa tamwimu hizo kuelekea maadhimisho ya siku ya idadi ya watu duniani Julai 11 mwaka huu ambapo kwa Tanzania maadhimisho hayo kitaifa yatafanyika Mkoani Mwanza.
Dkt. Dadi amesema hata hivyo vijana hao wanaotumia uzazi wa mpango ni wale walio mijini na wale wa vijijini wamekuwa wakikosa elimu sahihi ya namna ya matumizi bora ya uzazi wa mpango na hivyo kusababisha kuwepo kwa mimba nyingi za utotoni na wanafunzi wengi kukatisha masomo yao.