Monday , 31st Oct , 2016

Sekta ya usafiri ina jukumu kubwa katika maendeleo ya nchi, kwa kuwezesha wafanyakazi kufika kazini na bidhaa kufika sokoni.

Usafiri wa Trenia nchini Tanzania.

Licha ya umuhimu huo bado kuna changamoto kubwa kwa nchi na sekta nzima ya usafiri kutoa fursa ya usafiri salama, wa gharama nafuu na wa kuaminika.

Hayo ni kwa mujibu wa wataalamu wa kimataifa walioteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa, kutoa mapendekezo kwa ajili ya mifumo imara na bora zaidi kiafya.

José Viegas

José Viegas, ni mjumbe wa kundi hilo la usauri la ngazi ya juu kuhusu usafiri endelevu amesema umuhimu wa sekta ya usafiri ni uwezeshaji wa maendeleo, kupitia fursa inayotoa kwa watu na bidhaa, watu kwa kuwapeleka makazini, masokoni, maeneo ya umma

Viegas ameongeza changamoto zipo nyingi, hasa katika kutenga maeneo kwa magari binafsi, watembea kwa miguu na waendesha baiskeli haipewi uzito kama magari.