Wednesday , 19th Nov , 2014

Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA imebaini kuwepo kwa njama za kutaka kuondoa mjadala wa wizi wa zaidi ya Bilioni 321 fedha zilizokuwa katika akaunti ya Tegeta ESCROW Bungeni kwa kutumia chombo cha mahakama.

Akizungumza na waandishi wa habari mwanasheria wa UKAWA Mhe.Tundu Lissu amesema ipo taarifa ya barua kutoka mahakamani inayodai sakata la ESCROW liko mahakamani hivyo halipaswi kujadiliwa Bungeni na kusisitiza hakuna utaratibu wowote wa mahakama unaoipa mamlaka ya kulielekeza Bunge jambo la kufanya.

Kwa upande wake mwenyekiti mwenza wa UKAWA Mhe. James Mbatia amesema Bunge linahitaji muda wa kutosha kuhakikisha kashfa hiyo inajadiliwa kwa upana na baada ya uchunguzi wa Ripoti ya PAC kuonesha Bunge, watakaotuhumiwa kisiasa na kisheria wawajibishwe.

Jana, Naibu Spika wa bunge alikabidhi Ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kuhusu wizi wa zaidi ya shilingi Bilioni 321 fedha zilizokuwa katika akaunti ya Tegeta ESCROW ambao inadaiwa kuhusisha baadhi ya viongozi mbalimbali wa serikalini.