Monday , 23rd Jun , 2014

Umoja wa Katiba ya wananchi (UKAWA) umesema utaendelea na msimamo wao wa kutorejea kwenye Bunge Maalum la Katiba mpya mpaka yafanyike marekebisho ambayo watakubaliana nayo katika rasmu ya pili ya Katiba mpya.

Mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi - UKAWA Profesa Ibrahim Lipumba.

Akizungumza leo jijini Dar es-Salaam Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF, Prof. Ibrahim Lipumba amesema msimamo wao kwa sasa ni kuijadili rasimu ya Katiba mpya iliyotolewa na tume ya raisi na si vinginevyo.

Kwa upande wake nae Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe amesema kuwa lengo la umoja huo ni kupata Katiba iliyobora kwa wananchi pia hawataishia baada ya mchakato huo bali Ukawa itaendelea mpaka kwenye chaguzi zijazo.