Monday , 7th Nov , 2016

Gazeti la Ujerumani la Welt am Sonntag limeripoti kuwa wizara ya mambo ya ndani ya Ujerumani inataka wahamiaji kuzuiwa kufika katika nchi za Ulaya kupitia Bahari ya Mediteran, kwa kuwachukua baharini na kuwarejesha Afrika.

Boti ya wahamiaji ikizama bahari ya mediterainin.

 

Wizara hiyo inasema Umoja wa Ulaya unapaswa kuanzisha mfumo kama wa Australia ambao wahamiaji wanaookolewa baharini wanapelekwa katika kambi zilizoko katika nchi nyingine ambayo siko walikokusudia kufika.

Gazeti hilo limemnukuu msemaji wa wizara hiyo ya mambo ya ndani ya Ujerumani akisema mfumo huo utawafanya wahamiaji walio na azma ya kufika Ulaya kuvunjika moyo kuanza safari hiyo ya mashaka na iliyo hatari.

Pendekezo ni kuwapeleka wahamiaji wanaoanza safari zao katika nchi inayokumbwa na msukosuko ya Libya, hadi Tunisia, Misri au nchi nyingine za Kaskazini mwa Afrika.