Wednesday , 22nd Apr , 2015

Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema kuwa hakuna sababu kwa wanasiasa kutumia majukwaa ya kisiasa kueneza chuki wakati watanzania wakikabiliwa na matatizo mengi likiwemo tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana.

Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe .

Akihutubia maelfu ya wananchi wa manispaa ya Musoma mkoani Mara kiongozi huyo ACT wazalendo, amesema pamoja na watanzania kukabiliwa na matatizo makubwa, lakini anashangazwa na wanasiasa kushindwa kutumia majukwaa ya kisiasa katika kutatua changamoto hizo.

Aidha Bw Zitto, amejivunia mafanikio yake akiwa kama mbunge katika kilitetea taifa lake hasa katika kupambana na vitendo vya ufisadi na wizi wa fedha za umma huku akisema kamwe hawezi kutishika na siasa chafu zinazofanywa dhidi yake.

Kwa upande wake mwenyekiti wa taifa wa chama cha ACT Wazalendo bi Anna Elisha Mghwira, amesema kuwa chama hicho kimeanzishwa kwa lengo la kutetea maslahi ya taifa kwa kufuata mafundisho ya baba wa taifa hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere hasa kwa kutanguliza mbele uzalendo na uwajibikaji.