Sunday , 6th Dec , 2015

Mamlaka ya chakula na dawa TFDA kanda ya kati imezikamata na kuteketeza shehena ya bidhaa bandia na zilizokwisha muda wake wilayani Kilosa mkoani Morogoro

Baadhi ya bidhaa bandia picha na maktaba

Zoezi hilo la kuzikamata bidhaa hizo limefanyika katika kipindi cha kuanzia Novemba 30 hadi sasa katika maeneo ya Kilosa, Mikumi na Ruaha na katika zoezi hilo bidhaa ikiwemo vipodozi na vitu mbalimbali vilivyokwisha muda wake, bidhaa zilizoingizwa toka nje ya nchi kinyume na sheria zenye uzito wa nusu tani na thamani ya shilingi milioni 1.2,

Pamoja na vipodozi vyenye kemikali za sumu vilikamatwa na kuteketezwa ambapo mkaguzi wa chakula na dawa kanda ya kati Endybet Mbekenga ametoa wito kwa wafanyabiashara kutii sheria kwani kwa watakao bainika kurudia makosa hayo watafungiwa leseni zao sambamba na kufikishwa mahakamhani.

Kufuatia zoezi hilo, wananchi wa wilaya ya Kilosa wameeleza kufurahishwa na kuiomba serikali kuelekeza nguvu zake kuziba mianya ya uingizwaji wa bidhaa zisizofuata taratibu kwani wananchi wengi hawana elimu ya kutosha kuzibaini na zitaendelea kuwaumiza na kuwashauri wanawake kuacha matumizi ya vipodozi vilivyokatazwa.

Hata hivyo watanzania wenye dhana kwamba bidhaa hizo zinazo kamatwa hurudishwa madukani wameondolewa hofu kwa madai kuwa zimekuwa zikiteketezwa mbele ya wahusika.