Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya udhibiti chakula na dawa TFDA bwana Hiiti Sillo amesema mamlaka hiyo imeanza kufanya marekebisho ya sheria ya adhabu kwa watuhumiwa wa bidhaa bandia ili sheria hizo ziwe kali zaidi na mtu akibainika apewe adhabu kali.
Sillo ameyasema hayo kwenye mahojiani maalum na East Africa Radio nakusema sheria hiyo kama itapitishwa na Bunge itakua na meno zaidi yakuhukumu na faini kubwa sana hivyo itasaidia kupunguza uingizwaji wa bidhaa hizo ambazo zimekua na madhara makubwa kwa jamii inazozitumia.
Amesema mamlaka hiyo imeanza kushirikiana na mamlaka zingine duniani lengo likiwa ni kuhakikisha wanazuia bidhaa hizo kuanzia huko zinakozalishwa ili zisiendelee kusambazwa.
Sillo amewataka watumiaji kuacha kuwafisha wahusika wanaoingiza bidhaa hizo kwakua madhara yake ni makubwa na tayari ofisi yake imeweka maafisa wake mipaka yote ya nchi.





