Kutoka kulia ni Mfanyakazi wa Tewuta, Rashid Rajab, Mwanasheria Beatrice Monyo, Mwenyekiti Taifa wa Tewuta, Pius Makuke, Mwanasheria, Leila Farijalah.
Akiongea leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Taifa wa TEWUTA, Bw. Pius Makuke, amesema wamefikia uamuzi huo kwa sasa baada ya kuona kuwa Serikali kupitia mamlaka zake zinapuuzia malalamiko ya wafanyakazi katika kampuni za simu ambayo yameendelea kutolewa.
Bw. Makuke ameogeza kuwa endapo hata kilio chao kisiposikilizwa kupitia migomo ambayo watatangaza basi watafanya taratibu nyingine za kisheria ikiwemo kwenda mahakamani ingawa kwa sasa wametoa siku hizo 30 ili kusikilizwa maombi yao.
Mwenyekiti huyowa TEWUTA amebainisha kati ya mambo ambayo wanayapigania ikiwa ni pamoja na mikata ya kudumu katika makampuni ya sumu, uwasilishwaji mafao katika mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na ubaguzi kwa wafanyakazi wazawa.