Tuesday , 23rd Feb , 2016

Halmshauri ya Manispaa ya Temeke imeanza Ujenzi wa vyumba 10 vya madarasa katika shule ya msingi Maji Matitu ili kukabiliana na idadi kubwa ya wanafunzi katika shule hiyo ambayo imepokea idadi kubwa ya wanafunzi kuliko shule yoyote Dar es salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Saidi Meck Sadiki

Akizungumza katika ziara yake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Saidi Meck Sadiki amesema jumla ya vyumba 10 vitajengwa shuleni hapo huku wakiwa katika mchakato wa kujenga shule nyingine mbili mpya.

Mkuu huyo wa mkoa amesema zoezi hilo linakuja baada ya mutikio chanya wa serikali ya awamu ya tano na sera yake ya elimu bure ambapo amesema ili kuepuka adha ya wanafunzi wengi kukaa chini mkoa umejipanga kuboresha shule zenye idadi kubwa za wanafunzi.

Kwa upande wake mhandisi wa ujenzi huo Benjamini Maziku amesema kutokana na adha hiyo watajitahidi ambapo watakabidhi majengo hayo ndani ya miezi mitatu ijayo ili kuondoa adha ya wanafunzi hao.