Thursday , 29th May , 2014

Tume ya vyuo vikuu nchini Tanzania (TCU) imesema mfumo wa utambuzi wa gharama za masomo kwa kila mwanafunzi wa elimu ya juu upo tayari kwa ajili ya kuanza kutumika katika upangaji wa ada wa vyuo vya elimu ya juu vilivyopo nchini.

Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi nchini Tanzania, Dkt Shukuru Kawambwa.

Akiongea leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa ithibati na udhibiti wa TCU, Dkt Savinus Maronga amesema mfumo huo utatumika kama mwongozo kwa ajili ya serikali na taasisi za elimu ya juu katika kupanga na kukokotoa gharama za kuendesha programu za masomo hivyo kupata ada stahili.

Dkt. Maronga amesema mambo ya msingi yatakayozingatiwa katika mfumo huo ni pamoja na umiliki wa chuo, aina ya programu ya masomo, umri wa chuo na uwiano wa mwanafunzi na mwalimu ambapo TCU imejiandaa kutoa elimu na ushauri kwa vyuo vyote vinanvyohusika ili kufanikisha azma ya serikali ya kuhakikikisha watanzania wengi wanapata fursa ya kusoma elimu ya juu.