Tuesday , 1st Apr , 2014

Tume ya Vyuo Vikuu nchini Tanzania (TCU) imezindua rasmi mfumo wa kutathmini ada kwa vyuo vya elimu ya juu ambapo mfumo huo utasaidia kuondoa malalamiko kwa wanafunzi juu ya vyuo hivyo kujipangia ada vyenyewe.

Wanafunzi wa elimu ya juu wakiwa katika moja ya mahafali yaliyofanyika hivi karibuni

Kaimu Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Magishi Mgasa amesema mfumo huo utatumika pia kupanga rasmi viwango vya ulipaji ada kwa wanafunzi wa vyuo hivyo na kuondokana na vyuo vyenyewe kujipangia ada anayostahili mwanafunzi kulipa.

Profesa Mgasa amesema kuanzia mwaka wa fedha wa 2014 – 2015 vyuo vyote vya Elimu ya Juu nchini vitalazimika kupanga ada zao kwa kutumia mfumo huo na TCU itaendesha mafunzo kwa wakuu wa vyuo juu ya namna ya kuutumia mfumo huo.