Afisa wa Programu za jinsia katika shirika la Idadi ya watu la Umoja wa Mataifa UNFPA nchini Tanzania Ali Haji Hamad, amesema kuwa hali ya ukeketaji imepungua kutoka asilimia 18 mwaka 1996 hadi asilimia kumi mwaka jana.
Bw. Hamad amesema kuwa hata mikoa iliyokuwa inaongoza kwa matukio ya ukeketaji licha ya vitendo hivyo kuendelea lakini vimepungua kwa kiasi kikubwa mpaka kufikia karibu asilimia 50 tofauti na miaka ya nyuma.
Ulimwenguni kote inakadiriwa kuwa wanawake na wasichana milioni 200 wamekumbwa na ukeketaji na hivyo kuwaachia madhara ya kisaikolojia, kiafya na kijamii.


