Monday , 2nd Mar , 2015

Tanzania imekuwa ikipoteza mamilioni ya shilingi kutokanana vita zinazoendelea katika eneo la nchi za Maziwa Makuu kama vile Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Somalia na Sudani Kusini.

Akizungumza na East Africa Radio Mkurugenzi wa Taasisi inayojishughulisha na Utatuzi wa Migogoro ya kivita na Amani Cosmasi Bahali amesema serikali ya Tanzania inakosa kodi na tozo mbali mbali toka kwa wafanyabiashara wanaofanya biashara zao mipakani na nchi zenye migogoro kwa sababu ya vita hivyo.

Bahali ameongeza kuwa pia nchi inagharimika kwa kuchangia fedha nyingi kusaidia katika kutatua migogoro ambapo fedha hizo zingeweza kusaidia katika miradi mingine ya maendeleo.