Friday , 20th Mar , 2015

Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu, amewataka watalii wanaoingia Tanzania, kutumia ndege zinazotua moja kwa moja uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro na kuacha kutumia uwanja wa Jomo Kenyatta kwa muda mpaka muafaka baina yaTanzania na Kenya.

Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Tanzania, Mhe. Lazaro Nyalandu.

Agizo hilo amelitoa leo Jijini Arusha, mara baada ya kuvunjika kikao cha majadiliano ya sintofahamu ya zuio la Kenya dhidi ya magari ya utalii ya Tanzania kuingia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyata na kikao kilishirikisha wataalamu wa wizara ya utalii wa nchi hizo, Afrika Mashariki naViwanda na Biashara, ambapo kilivunjika jijini Arusha.

Kikao hicho kilifanyika kama agizo la Mawaziri wa nchi hizombili, ambapo waliagiza wataalamu wajadiliane mambo yote yaliosababisha zuio hilo, kabla hayajafika kwa Mawaziri, lakini kikao kikawa kigumu kukukubaliana ajenda moja tu ya kwa nini Jamuhuri ya Kenya walizuia magari ya Tanzania wakati hawajawahi kubadilisha makubaliano hayo.

Moja ya makubaliano ya mkataba huo wa mwaka 1985, ulikuwa unasema jinsi ya kudumisha ushirikiano katika biashara ya utalii na pia waliweka bayana magari yote ya Kenya, yataruhusiwa katika mipaka iliyo wazi Tanzania na kupeleka watalii Arusha, Musoma, Moshi na Tanga, na pia magari ya Tanzania yanayopeleka wageni Kenya, yataruhusiwa kuingia katika miji yote ya jamuhuri ya Kenya na hayajawahi kubalishwa makubaliano hayo.

Amesema baada ya kutokea tatizo hilo mawaziri waliagiza kukaa kikao kifanyike Tanzania Machi 19 na kushirikisha Wataalam wa Wizara ya Utalii wa nchi hizo, Afrika Mshariki na Viwanda na Biashara, ili wajadiliane sababu ya zuio hilo na ajenda ilikuwa hiyo tu, wakati hawajawahi kubadilisha mkataba huo na matokeo yake kikao kilivunjika.

Nyalandu amesema kikao kilivunjika sababu kila upande unavutia kwake Tanzania inataka kuelezwa sababu ya zuio hilo, huku Kenya wakisema hilo siyo la muhimu kwao, bali la muhimu ni kufanya marekebisho la mkataba uliopo wa masuala ya utalii wa mwaka 1985.

Makatibu wa Tanzania walitaka ajenda kuu katika kikao hicho kiwe ni zuio la magari ya Tanzania kuingia Jomo Kenyatta na wao hawakutaka wanataka ajenda ya kuongelea marekebisho au maboresho ya mkataba ambao haujawahi kuvunjwa wala kurekebishwa tangu mwaka 1985.

Amesema baaada ya sintofahamu hiyo kikao kilivunjika na kesho yake (Jana) ilitakiwa kikao cha mawaziri kifanyike nacho hakikufanyika kwa ajili ya sintofahamu hiyo. Aidha kutokana na hilo Nyalandu amesisitiza wageni wote wanaoingia Tanzania watumie uwanja wa KIA badala ya Jomo Kenyatta mpaka hapo watakapoelewana.

Sintofahamu hiyo ilikuja tangu Desemba 22 mwaka jana 2014, baada ya Jamuhuri ya Kenya kuzuia magari ya watalii yanayotoka Tanzania kutoingia uwanja w akimataifa wa Jomo Kenyatta, wakati kuna makubalino ya tangu mwaka 1985 na hayajawahi kufutwa.