Mratibu Kiongozi Maonyesho ya kimataifa ya Utalii Samwel Dia.
Maonesho hayo ya 15 ya utalii, yana adaliwa na chama cha mawakala wa utalii nchini TATO.
Katika viwanja vya Magereza Kisongo Arusha Mratibu Kiongozi Maonesho hayo Samwel Dia ameeleza kwamba maandalizi yote kwaajili ya maonesho yamekwishakamilika na tayari waoneshaji wanakamilisha hatua za mwisho za kuingiza bidhaa zao katika eneo hilo.
Mratibu huyo ameongeza kwamba makampuni ya utalii, mahoteli, mashirika ya ndege yameshakamilisha taratibu zote za ushiriki na kwamba kinachosubiriwa ni kuanza rasmi kwa maonesho.
Meneja wa Karibu TMT, Nakaaya Sumari amesema takribani wageni elfu nane kutoka kona mbalimbali za dunia wanatarajiwa kutembelea maonesho hayo na hiyo kuwa fursa ya kipekee ya kuutangaza utalii wa Tanzania huku baadhi ya washiriki wakieleza matumaini ya kukuza biashara zao kupitia maonesho ya (KTMT).
Maonesho haya yanatajwa kutoa fursa murua kwa watanzania kutangaza utalii wao kwa wageni kutoka nchi za Ulaya, Marekani, Asia na kwingineko pamoja na kujifunza masuala mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara wengine watakaofika hapa nchini.