Akizungumza mjini Morogoro Mratibu wa Kituo hicho Prof. Eliakim Zahabu, amesema ujenzi wa kituo hicho umefadhiliwa na serikali ya Norway kwa gharama za dola za Marekani 100,000.
Prof. Zahabu amesema misitu ni biashara inayoshamiri duniani na kwa takwimu zilizopo nchi inaweza kupata faida kubwa katika biashara ya hewa ya ukaa kutokana soko hilo kuwepo Umoja wa Mataifa.
Amesema kazi kubwa ya kituo hicho ni kuratibu upimaji,uwasilishaji na ukahikiki wa takwimu za kaboni kwa niaba ya serikali na ili kutimiza jukumu hilo na mengine na kituo kitahuisha sekta zingine zinazofanya kazi hiyo.
Aidha, mratibu huyo ameongeza kuwa kituo hicho kitahusika kutoa ushauri wa namna ya upimaji, uwasilishaji na uhakiki wa takwimu ili kulinda maslahi ua jamii na mzingira katika masuala ujumla.