Tuesday , 29th Nov , 2016

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sihaba Nkinga amesema Tanzania ni nchi pekee barani Afrika ambayo imechaguliwa kama nchi ya kuigwa kwenye juhudi za dunia kupambana ukatili wa wanawake na watoto.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sihaba Nkinga

Bi. Nkinga ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa mashauriano wa kanda ya Afrika kuhusu Mtandao wa Kuzia Unyonyaji  na Usafirishaji  wa Watoto ambapo amesema Tanzania inapata sifa hiyo kutokana na kuridhia kutekeleza mikataba mbalimbali ikiwemo kutunga sera na sheria pamoja na  mikakati ya kupambana na ukatili dhidi ya watoto.

Aidha amezitaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wa kufanya tafiti za ukatili dhidi ya  wanawake na watoto barani Afrika ambapo amezitaja nchi nyingine zinazotajwa kuwa mfano wa kuigwa kuwa ni pamoja na Mexico, Indonesia na Sweden.