Kauli hiyo imetolewa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Onesmo Sanga, alipokuwa akiongea katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii ofisini kwake.
Dkt. Sanga amesema Tanzania nzima ina madaktari bingwa wa figo 10 tu, hali inayosababisha gharama za matibabu hayo kuwa kubwa, na kuwafanya Watanzania wengi kushindwa kumudu gharama na kusababisha kupoteza maisha kwa wagonjwa wa ugonjwa huo.
Licha ya uhaba huo Dkt. Sanga amesema pia wanakabiliwa na changamoto kubwa ya vifaa tiba, ilicha ya kuwa kuna baadhi ya hospitali za serikali hapa nchini ikiwemo ya Rufaa ya Mbeya na hospitali ya Mkoa Dodoma, hutoa huduma ya kusafisha damu.
