Saturday , 15th Mar , 2014

Serikali ya Tanzania imetumia shilingi bilioni 500 katika utekekezaji wa miradi ya matokeo makubwa sasa BRN katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2013.

Kiongozi wa BRN wa wizara ya fedha Emmanuel Tubuka aliwaambia waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam kuwa serikali imefanikiwa katika kutekeleza miradi mbali mbali chini ya mpango wa BRN ambapo alitaja miradi hiyo kuwa ni Elimu iliyopewa shilingi bilioni 8.3 na miradfi ya maji shilingi bilioni 86.

Tubuka alitaja miradi mingine kuwa ni ya Kilimo shilingi bilioni shilingi bilioni 10.2, shilingi bilioni 146.6 miradi ya uchukuzi na shilingi bilioni 339.4 kuimaruisha sekta ya nishati.