Wednesday , 2nd Dec , 2015

Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara (UNCTAD) limesema Tanzania bado inatatizo kubwa la umaskini wa wastani wa asilimia 28.2 huku maeneo ya vijijini yakiwa ndiyo yameathirika zaidi.

Akitoa matokeo ya tafiti uliofanyika katika nchi 48 duniani, Mtafiti Mshiriki Dkt. Osward Mashindano amesema kuwa vikwazo vinavyochangia taifa kutofikia malengo ya Milenia ni ukosefu wa rasilimali za kuwawezesha wananchi kufanya shughuli zao za kila siku, njia za uzalishaji bado ni ndogo hasa maeneo ya vijijini na ukosefu wa uelewa.

Ameshauri kuwa njia sahihi yakupambana na umaskini ni lazima serikali ihakikishe kuwa na uhakika na vyanzo vyake vya mapato na kuziwezesha kifedha Halmashauri zote nchini na kuzisimamia katika uendeshaji wa mapato yake..

Kwa upande wake Kamishna msaidizi Wizara ya Fedha za Nje nchini Jerome Burreta amesema kuwa serikali tayari imeanza kushughulikia tatizo la umaskini kwa kuboresha miundombinu hasa maeneo ya vijijini na yenye matatizo yanayochangia umaskimi nchini.