Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi. Jacqueline Maleko, amesema uanzishwaji wa matumizi ya Made in Tanzania yataongeza imani ya wateja juu ya bidha na huduma zinazozalishwa Tanzania, hatua itakayopanua wigo wa masoko ya bidhaa na huduma husika.
Bi. Maleko amesema nchi za China, Marekani, Uingereza na Italia zimefanikiwa kibiashara kwa kutumia hatua kama hiyo, na kwamba TANTRADE itahakikisha kampuni na biashara zote za kigeni zinailipa Tanzania pale zitakapotumia maneno hayo na alama za Made in Tanzania.
Bi. Maleko ametaja baadhi ya alama hizo kuwa ni pamoja na vivutio maarufu ambavyo havipatikani sehemu yoyote isipokuwa Tanzania, vivutio kama mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama na alama nyingine zinazoitambulisha Tanzania.