Thursday , 19th Mar , 2015

Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye amesema kuwa mfumo wa elimu uliopo nchini haumwezeshi kijana wa Kitanzania kushindana kwenye soko la ajira la Afrika Mashariki.

Waziri mkuu wa zamani katika awamu ya tatu Fredick Sumaye.

Sumaye ameyasema hayo leo kwenye mkutano wa wamiliki na mameneja wa shule na vyuo binafsi nchini uliofanyika mjini Dodoma.

Amesema hata madaraja ya ufaulu yanayotolewa na Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi yanawachanganya wananchi kwani alama alizotakiwa kupata mwanafunzi aliyefeli kwa sasa ni alama za ufaulu.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii, Magreth Sitta amesema serikali inathamini mchango mkubwa unaotolewa na shule za watu binafsi katika kukuza sekta ya elimu nchini.

Amewataka wamiliki wake kushirikiana kwa karibu na serikali ili kwa pamoja waweze kuinua sekta ya elimu nchini.