Akizungumza na www.eatv.tv, sugu amesema muitikio umekuwa mkubwa lakini bado hajaipata picha husika, na kusisitiza mtu yeyote atakayeipata picha hiyo amtumie kwa email na atapewa zawadi yake, huku akiahidi kuweka usiri mkubwa kati yao.
“Kwa kweli bado mpaka sasa hivi sijampata, najua wanakataza kupiga picha jela ndio maana nimetoa tangazo kama kuna mtu anayo, na sitamtaja, na ndio maana tunataka kwa njia ya email, ninachotaka ni picha kwa ajili ya kukamilisha kitabu chetu”, amesema Sugu.
Sugu ameendelea kwa kusema kwamba, ”muitikio umekuwa mkubwa lakini picha bado hatujaipata, inanitia moyo watu wanataka kushiriki katika kukamilisha hiki kitabu, hii hata kama ni askari jela alinipiga picha kwa mizuka yake, nao wanaruhusiwa kutuma ile picha kwenye email yangu ambayo ni [email protected] na hatutamtaja”.
Hivi karibuni Mbunge huyo aliandika ujumbe mfupi kwenye ukurasa wake wa twitter akimtaka mtu mwenye picha yake akiwa amevaa sare za jela amtumie kwa ajili ya kumalizia kurasa ya mwisho 'cover' ya kitabu chake cha 'SIASA NA MAISHA, na kuahidi kumpatia kiasi cha sh milioni 1 yeyote atakayefanikisha kuipata picha hiyo.
