
Aliyekuwa rais wa Tanganyika Julius Nyerere (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na rais wa Zanzibar Abeid Aman Karume
Msekwa na Masoud jana waliitwa na kuhojiwa na kamati Na. 2 ya Bunge Maalum la katiba. Akizungumza na waandishi wa Habari mwenyekiti wa kamati hiyo Shamsi Vuai Nahodha alisema kuwa wajumbe wa kamati yake ambao walikuwa wakijadili sura ya kwanza na ya sita ya Rasimu ya Katiba zinazohusu Muungano, walitilia shaka na kuzua mabishano makali juu ya mambo makuu matano.
Mambo hayo yalitajwa kuwa ni kusainiwa kwa mkataba wa Muungano baina ya Julius Nyerere na Shekh Abeid Aman Karume, kuridhiwa kwa mkataba wa muungano na baraza la mapinduzi , muundo wa muungano uliopendekezwa kwenye mkataba wa muungano , namna jina la Tanzania lilivyopatikana wakati sheria ya kuridhia muungano imetaja Tanganyika na Zanzibar na utata wa Saini ya Nyerere na Msekwa kwenye Muungano.