Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonald Paulo
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonald Paulo amesema shehena hiyo ya vipodozi imekamatwa eneo la modeco mjini Morogoro ikiwa inashushwa kutoka kwenye lori tupu la mafuta ya petrol, lililokuwa likitoka Zambia kupitia mpaka wa Tunduma, aina ya track tanker namba T927 CHX, na tela namba T692 CJE.
Vipodozi vilivyokamatwa ni pamoja na Betasal, Diproson, Citro Light na Top Lemon ambapo kamanda huyo wa polisi ameahidi kushirikiana na mamlaka ya mapato nchini TRA, na TFDA, sambamba na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa tukio hilo.
Jumamosi mamlaka ya chakula na dawa kanda ya kati iliteketeza shehena ya madawa na vipodozi bandia, vyenye kemikali za sumu na vilivyoingia nchini kinyume na sheria katika wilaya ya Kilosa baada ya msako mkali kwenye maeneo ya ruaha, Kilosa na Mikumi, na kuwaonya wananchi kuacha kutumia bidhaa hizo, huku wakiwaonya pia wafanyabiashara wanaoingiza kinyemela bidhaa hizo.