
Wito huo umetolewa mara baada ya tafiti ya miaka miwili ijulikanayo kama Kiufunza iliyofanywa na taasisi ya Twaweza kwa kushirikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) pamoja na shirika la innovations for poverty action IPA katika shule 350 nchini.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uwasilishwaji wa ripoti hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza Bw. Aiden Eyakuze amesema asilimia 93 ya waalimu wanapendekeza malipo kwa utendaji bora yawekwe kwenye mtaala wa kimataifa ili kuwapongeza walimu katika kila hatua wafanyapo kazi nzuri.
Eyakuze ameshauri ili kuondoa asilimia 47 ya waalimu ambao wanafanya shuguli zingine katika muda wa kujifunzia na kupelekea wanafunzi kukosa mafunzo katika muda uliopangwa ni vyema serikali ikaweka utaratibu wa kuwafanya waalimu wawajibike.