Wednesday , 22nd Jul , 2015

Serikali imetakiwa kuangalia upya ushuru wa mabasi ya kwenda mikoani ambapo huenda Ukasababisha Nauli za Mikoani kupanda maradufu.

Mabasi ya Abiria yakiwa yamepaki katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo Terminal

Wakizungumza na East Africa Radio wamiliki wa mabasi wamesema serikali imepandisha ushuru toka 10% hadi 25% sawa na shilingi million 42 mpaka milion 92 ikiwa ni ongezeko la million 50 kwa kila basi moja.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi TABOA Ernea Mrutu amesema kupanda huko kwa ushuru kutasababisha nauli za mabasi ya kwenda mikoani kupanda maradufu huku wakimtaka waziri wa Fedha Bi. Sada Mkuya kujibu maombi yao ya kutaka kupunguziwa kwa ushuru huo ili ubaki wa 10%.

Kwa upande wa mwakilishi toka SUMATRA David Mziray amesema watasikiliza hoja zote na kuwashauri namna nzuri ya kufanya ili serikali iwapunguzie ushuru huo ambapo wananchi wa kawaida ndiyo watakaoathirika baada ya bei kupanda.