Monday , 19th Jan , 2015

Mamlaka za nchi zatakiwa kuwa makini katika utoaji wa vibali vya wageni wanaoishi nchini ili kupunguza uwezekano wa kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watu wasio na sifa.

Waziri wa Kazi na Ajira Gaudensia Kabaka

Sekretarieti ya ajira nchini Tanzania imezitaka mamlaka nyingine za serikali kuwa makini zinapotoa vibali vya hati ya kuishi nchini pamoja na vyeti vya kuzaliwa ili kuepusha watu wasio na sifa hususani wageni kuajiriwa serikalini.

Katibu msaidizi wa sekretarieti ya ajira nchini Bw Malimi Muya ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akiongea na hotmix ilipotaka kufahamu kuhusu tuhuma za raia wakigeni kuajiriwa serikalini.

Bwana Muya ameongeza kuwa Ofisi yake inahimiza vijana walioko vyuoni na mashuleni kuchukua masomo ya sayansi na Technolojia kwakua kwa sasa fani hiyo ndiyo yenye soko kubwa la ajiri duniani.