
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Dkt Godfrey Simbeye (katikati) akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni Bw. Abdulsamad Abdulrahim, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Pietro Fiorentini.
Taasisi hiyo imesema kuwa kupatikana kwa mradi huo siyo tu kutainufaisha nchi kiuchumi bali kunatoa fursa pana ya ushiriki wa wazawa katika miradi mbalimbali ya uwekezaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Dkt. Godfrey Simbeye, ametoa pongezi hizo Jijini Dar es Salaam leo na kutaja moja ya faida kubwa za mradi huo kuwa ni ajira za moja kwa moja zaidi ya elfu thelathini, soko kwa viwanda vya vifaa vya ujenzi huku bandari ya Tanga ikinufaika na shilingi bilioni 1.2 zitakazotokana na upanuzi utakaoiwezesha kusafirisha tani za ujanzo laki tano za mabomba na vifaa vitakavyotumika kwenye mradi huo.
Mdau muhimu wa TPSF katika mradi huo ni kampuni ya Pietro Fiorentini ambayo kwa kiasi kikubwa ndiyo ilianzisha mazungumzo na serikali ya Uganda juu ya upatikanaji wa mradi huo.