Thursday , 8th May , 2014

Serikali ya Tanzania imesema mishahara ya walimu imechelewa katika baadhi ya mikoa kutokana na matatizo ya kibenki yaliyojitokeza na si ucheleweshaji uliofanywa na serikali.

Waziri wa fedha na uchumi wa Tanzania Bi.Saada Mkuya Salum.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha na Uchuni Mhe. Saada Mkuya wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbozi magharibi, Mhe David Silinde aliyetaka kufahamu kwa nini mishahara hiyo imechechelwa licha ya watumishi wa umma kutakiwa kulipwa tarehe 25 ya kila mwezi.

Kwa mujibu wa waziri Mkuya, serikali ilishatoa fedha za mishahara kwa watumishi wake tangu April 24 mwaka huu na kwamba kilichotokea ni ucheleweshaji uliofanywa na benki.