Tuesday , 10th Jun , 2014

Serikali ya Tanzania imebainisha kuwa suala linalolalamikiwa na baadhi ya wabunge la kutopewa ulinzi na serikali sio la kiserikali bali ni la muhimili wenyewe kuamua kupendekeza sheria ya aina hiyo katika sera zake.

Waziri wa nchi, ofisi ya waziri mkuu (sera, uratibu na bunge) William Lukuvi.

Akiuliza swali katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini Dodoma, Mbunge wa Muhambwe, Mhe. Felix Mkosamali, alitaka kufahamu kwa nini serikali inatoa ulinzi kwa baadhi ya viongozi wake wa juu na kuwasahau wabunge ambao wakati mwingine wako kwenye hatari zaidi.

Akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri Mkuu, Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Uratibu na Bunge Mhe. William Lukuvi amesema kuwa, suala hilo lipo ndani ya muhimili wenyewe kufanya mapendekezo na si juu ya serikali.