Tuesday , 21st Jun , 2016

Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini Daniel Nswanzingwanko ameeleza Bungeni Dodoma adha ya maji wanayokumbana nayo wakazi wa Kasulu na kuitaka serikali itoe tamko juu ya ahadi zake za maji kwa wakazi wa mji wa Kasulu.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Isack Kamwele amesema serikali imetenga milioni 200 kwa ajili ya kuboresha huduma ya maji mjini Kasulu.

Serikali imesema pia imekamilisha usanifu wa mradi mkubwa wa maji utakaosaidia wananchi wa Kasulu na kata zake ambapo andiko la mradi huo limeshakamilika.

Naibu Waziri Kamwele amesisitiza kuwa juduma ya maji kupitia mradi huo ambao utagarimu dola milioni 9.9 ambazo ni mkopo ambao unatarajiwa kupatikana kutoka benki ya watu wa India.

Aidha Mbunge Nswanzigwanko ameiuliza serikali kama fedha hizo zisipotoka wananchi watarajie nini,? Waziri Kamwele akajibu kwamb serikali ya awamu ya tano imejipanga vyema kutatua kero za wananchi kwa kukusanya kodi kila kona.