Wednesday , 1st Jun , 2016

Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo yaanza kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele nchini.

Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Ayoub Magimba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati akifungua mkutano wa mwaka wa mapitio wa mpango wa Taifa wa kudhubiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele nchini.

Profesa Magimba amesema mkutano huu unawakutanisha waratibu kutoka mikoani na wadau nje ya nchi na lengo la kuangalia utekelezaji na changamoto zilizowakabili wakati wa utekelezaji wa mikakati na malengo waliyojiwekea mwaka uliopita na vilevile kuweka malengo kwa mwaka ujao wa fedha.

Amesema wizara imeweka kipaumbele kwa kuwapatia wananchi elimu,kinga na tiba na hivyo kuyaingiza kwenye mkakati wa Taifa wa Afya wa tatu ulioisha na mkakati wa Taifa wa afya wa nne ulioanza mwaka 2015 hadi 2020.

Naye Mratibu wa Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt.Upendo Mwingira alisema,tathimini ya mwaka 2,000 zinaonesha magonjwa hayo yapo karibu halamashauri zote nchini hususan ukanda wa Pwani kuna wagonjwa wengi wa Matende na Mabusha, Trakoma.

Maambukizi zaidi ya asilimia 30 yapo maeneo ya wafugaji, minyoo ya tumbo upo kila mahali kutokana na shughuli za kila siku za binadamu kupitia udongo na vyakula, maeneo ya ziwa kuna maambukizi mengi kwa ugonjwa wa kichocho hususan kwa watoto na ugonjwa wa usubi unaothiri zaidi ngozi inapatikana mkoa wa Morogoro.