Thursday , 8th May , 2014

Wizara ya Mambo ya Ndani nchini Tanzania, imezungumzia tukio lililotokea jana mkoani Mwanza ambapo mtuhumiwa wa kesi ya mauaji alivua nguo kama ishara ya kupinga kuchelewesa kusikilizwa kwa kesi inayomkabili.

Maofisa wa polisi wakiwa wamemshikilia mtuhumiwa wa kesi ya mauaji anayedaiwa kuvua nguo hadharani mkoani Mwanza jana, akiishinikiza mahakama iharakishe kusikiliza kesi inayomkabili.

Mkurugenzi wa Idara inayoshughulikia malalamiko ya wizara hiyo, Bw. Augustine Dominic Shio amezungumzia suala hilo leo wakati akiongea na East Africa Radio na kufafanua kuwa tukio hilo na mengine ya aina hiyo
yanachangiwa na kuchelewa kupatikana kwa ushahidi zinazowakabili watuhumiwa.

Kwa mujibu wa Shio Idara yake inafuatilia tukio hilo na mengine yote ili kuhakikisha haki za binadamu hususani zile za walio katika vizuizi zinafuatwa.