Wednesday , 16th Mar , 2016

Katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Desemba 2014 jumla ya kesi 8,436 za dawa za kulevya zilifunguliwa katika mahakama mbalimbali hapa nchini.

Waziri wa Ofisi ya waziri Mkuu sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu nchini Jenister Muhagama

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Ofisi ya waziri Mkuu sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu nchini Jenister Muhagama wakati akipokea na kujadili Taarifa ya Serikali kuhusu hali ya sasa katika uthibiti wa matumizi ya dawa za kulevya pamoja na mafanikio,changamoto na matarajio yaliyopo kutoka Kamati ya Bunge ya Kudumu ya masuala ya Ukimwi.

Waziri huyo wa ofisi ya Waziri Mkuu ameongeza kuwa kati ya kesi hizo kesi 3,577 zilianza kusikilizwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika ambapo kesi 754 zimeshatolewa hukumu

Aidha Mhe Mhagama amesema katika kudhibiti hali hiyo Katika kuhifadhi vidhibiti vya dawa za kulevya nchini Serikali imeanza Ujenzi wa ghala la kuhifadhi vielelezo vya dawa za kulevya,liko katika Ofice za Kitengo cha kudhibiti Dawa za Kulevya cha Jeshi la Polisi na ujenzi umeshakamilika,na hilo ghala hilo limepunguza tatizo la ukosefu wa mahali pa kuhifadhi dawa za kulevya zinazokamatwa.