Thursday , 4th Jun , 2015

Serikali imeshauriwa kuwashirikisha wafanyabiashara wadogo ambao ndiyo wengi hapa nchini ili kuwa na uchumi unaokua tofauti na ilivyo sasa.

Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya utafiti wa masuala ya umasikini nchini Tanzania REPOA Profesa Samwel Wangwe ameishauri serikali kuwashirikisha wafanyabiashara wadogo ambao ndiyo wengi hapa nchini ili kuwa na uchumi unaokua tofauti na ilivyo sasa wengi wa wafanyabiashara hao wameachwa wakijiendesha wenyewe.

Akizungumza jijini Dar es salaam katika kongamano la wanawake wafanyabiashara wa sokoni nchini Tanzania Profesa Wangwe amesema athari za kutowashirikisha wafanyabiashara hao ni kukua kwa uchumi ambao hauwashirikishi wananchi wengi.

Profesa Wangwe amesema mhango wa sekta isiyo rasmi iwapo watashirikishwa ni mkubwa hivyo ni vyema sasa serikali ikaanza kuchukua hatua ya kuhakikisha inashirikisha sekta hiyo ili kuwa na uchumi mkubwa zaidi.

Amesema sekta ya wafanyabiashara hapa nchini ndio imekuwa ikitoa ajira nyingi si wanawake pekee bali pia kwa vijana wengi na hivyo kusababisha kukidhi mahitaji yao ya kiuchumi na kuachana na dhana ya kuitegemea serikali katika kuwaajiri.