Tuesday , 27th May , 2014

Vitendo vilivyokatazwa vya uuzaji damu katika hospitali za umma nchini Tanzania bado vinaendelea licha ya kiwango kidogo cha damu kinachokusanywa kupitia mpango wa taifa wa damu salama.

Rais wa klabu za waandishi wa habari nchini Tanzania, Kenneth Simbaya.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa tiba asilia kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Paulo Mchome katika mkutano baina ya uongozi wa mpango wa taifa wa damu salama na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini, mkutano unaoangalia namna viongozi wa dini wanavyoweza kushawishi waumini wao kuchangia damu kwa hiari.

Kwa upande wake, Rais wa Klabu za Waandishi wa Habari Bw. Kenneth Simbaya amesema bado vyombo vya habari havijatekeleza jukumu lake la kuandika na kutoa habari ambazo zitachochea jamii kuchangia damu kwa hiari hatua aliyosema inaweza kusaidia kuokoa maisha ya wagonjwa wanaopoteza maisha kwa ukosefu wa damu.