Wednesday , 30th Apr , 2014

Serikali ya Tanzania imetakiwa kutoa mafunzo ya uzalendo na uadilifu kwa wanafunzi wanaosomea fani za fedha ili kuepusha vitendo vya wizi na ubadhirifu wa fedha uliokithiri katika sekta hiyo kwa sasa.

Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wamesema hayo katika mahojiano na East Afrika Radio ambapo wamesema elimu ya uadilifu na uzalendo itawafanya watambue umuhimu wao na kazi yao kwa maendeleo ya taifa.

Mmoja wa wanafunzi hao ni Waziri wa Elimu wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho Ezra Mathew ambaye amesema matukio ya ubadhirifu yanayoshuhudiwa hivi sasa sio ajali bali ni matokeo ya wakufunzi wa fani za fedha kutokuwa na uzalendo pamoja na uadilifu wa kusimamia rasilimali za nchi pamoja na za wateja wanaowahudumia.