Tuesday , 22nd Mar , 2016

Mhifadhi Mkuu wa Mbuga ya Serengeti Wiliam Mwakilema amesema kuwa Nyumbu wanaohama hama kutoka mbuga hiyo kwenda masai mara nchini Kenya ni watanzania hivyo kusiwepo na upotoshaji wowote utakaolenga kujinufaisha kibiashara.

Mhifadhi Mkuu wa Mbuga ya Serengeti, Wiliam Mwakilema

Mhifadhi Mkuu wa Mbuga ya Serengeti Wiliam Mwakilema amesema kuwa Nyumbu wanaohama hama kutoka mbuga hiyo kwenda masai mara nchini Kenya ni watanzania hivyo kusiwepo na upotoshaji wowote utakaolenga kujinufaisha kibiashara.

Akizungumza na Waandishi wa Habari waliofanya ziara ya kutembelea Mbuga hiyo iliyoratibiwa na Tanapa, Mhifadhi huyo amesema kuwa kundi la Nyumbu wanaokadiriwa kufikia milioni 1.5 huama kipindi cha mwezi Novemba na Desemba kila mwaka hutembea hadi nchini Kenya.

Mhifadhi huyo amesema kuwa nyumbu hao asili yao ni Tanzania kwani hubeba mimba na kuzaa wakiwa nchini Tanzania na husafiri hadi nchini Kenya kutembea kama sehemu ya ikolojia ya wanyama hao hivyo jambo hilo lisichukuliwe vibaya na nchi jirani.

Aidha, amewataka watanzania hususani waajiri na wafanyakazi kutenga muda wa kutembelea mbuga hizo kama sehemu ya kujifunza, kupumzika na kujiburudisha kutokana na vivutio vilivyopo na mandhari nzuri Ikiwa ni pamoja na kuvilinda vivutio hivyo kwa faida ya vizazi vilivyopo na vile vijavyo.

Kundi kubwa la Nyumbu kutoka Mbuga ya Serengeti huama kila mwaka na kuelekea nchini Kenya ambako hurejea nyumbani kwao Tanzania baada ya miezi miwili hadi mitatu.