Tuesday , 26th May , 2015

Serikali imesema kuwa inathamini mchango mkubwa unaotolewa na sekta binafsi katika kutoa ajira kwa vijana na kusema kuwa itarasimisha sekta hiyo ili iweze kutoa ajira kwa wingi kwa kundi hilo kwani ndiyo mhimili mkuu wa ajira nchini.

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia kabaka

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia kabaka wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma wakati akitoa tathmini ya awali ya hali ya nguvukazi na ajira nchini.

Kabaka amesema kuwa kwa kipindi cha Januari na Machi mwaka huu sekta binafsi imetoa jumla ya ajira 64,331 ambayo ni sawa na asilimia 95.4 ya ajira zote zilizotolewa kwa kipindi hicho ukilinganisha na upande wa serikali ambayo kwa kipindi hicho hicho imetoa jumla ya ajira 4,363 sawa na asilimia 6.4.

Kwa upande wake katibu mkuu wa Wizara ya Kazi na Ajira, Eric Shitindi amewataka wadau mbalimbali wa sekta binafsi nchini kutambua kuwa jukumu la kutoa ajira kwa vijana siyo la serikali peke yake bali ni la kila mtu.