
Wanafunzi
Dkt. Msonde ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza matokeo ya kidato cha pili na darasa la nne kwa mwaka 2018, ambapo amesema wanafunzi katika mtihani huo 452,273 sawa na asilimia 89.68 wamefaulu.
Aidha amesema wanafunzi 52,073 wameshindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na masomo ya kidato cha tatu.
Kuhusiana na matokeo ya darasa la nne kati ya watahiniwa 1,302,461 wa darasa la nne waliofanya mtihani huo sawa na asilimia 95.58, waliofaulu kwa kupata daraja A, B, C, na D ni 1,213,132 sawa na asilimia 93.16.
"Ubora wa ufaulu umezidi kuimarika kwa kuwa watahiniwa waliofaulu kwa daraja A,B na C umeongezeka kwa asilimia 0.03 ikilinganishwa na mwaka 2017,”amesema Dkt. Msonde."