Monday , 21st Jul , 2014

Mbinu zilizopitwa na wakati katika kilimo, uhuru wa masoko yasiyo na ubora na viwango na ukosefu wa elimu imeelezwa kuwa ndio sababu ya kushuka kwa soko la ushindani kwa Tanzania katika Afrika Mashariki.

Waziri wa Viwanda na Biashara nchini Tanzania Dkt Abdallah Kigoda.

Hayo yamebainshwa na wadau wa biashara ya mazao ya nafaka nchini wakati wa majadiliano ya wadau hao yaliyoandaliwa na Baraza la nafaka la ukanda wa Afrika Mashariki EAGC.

Mwakilishi kutoka kituo cha uhamasishaji wa biashara, ukanda wa nchi za Afrika Mashariki wa shirika la misaada la marekani, Isaack Tallam amesema tatizo sio wakulima bali ni wafanyabiashara wa kati.